Jinsi ya Kuandika Tangazo| O level na Advance
Matangazo ya gazetini huandikwa
kwa lengo la kutangaza biashara. Kwa kuwa magazeti yana wasomaji lukuki, hivyo
njia hii hudhaniwa kuwa miongoni mwa njia rahisi zaidi za kuwafikia watu wengi
ambao hapo baadaye hugeuka wanunuzi wa bidhaa inayotangazwa.
Uandishi mzuri zaidi wa matangazo
ndiyo utakaofanya bidhaa yako inunuliwe. Uandishi mbovu hugeuka kero kwa watu.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
1. Kichwa cha habari. Kiandikwe kwa herufi kubwa.
2. Taja aina ya biashara.
3. Taja bidhaa unazouza na bei zake.
4. Taja mahali inapopatikana bidhaa yako.
5. Taja mawasiliano yako. Mawasiliano yanaweza kuwa ya
simu, barua n.k. hata hivyo, simu ni
bora zaidi, kwa sababu
mawasiliano yake ni ya haraka.
Mfano wa Kwanza
MASOMO KWA WANAFUNZI WOTE
Kituo cha Mwalimu Makoba kinatoa
huduma ya kufundisha wanafunzi wanaorudia mitihani na walio shuleni kwa masomo
ya sayansi, sanaa na biashara. Gharama zetu ni shilingi 300,000/= tu kwa mwaka
mzima.
Kituo hiki kinapatikana Kinondoni
Manyanya mkabala na shule ya sekondari Kambangwa.
Mawasiliano:
0754 89 53 21
0653 25 05 66
Mfano wa Pill
Jifanye wewe ni afisa habari wa shirika la ndege Tanzania, andika tangazo kwa abiria kuhusu katizo la usafiri wa ndege namba TY JET 343 iliyokuwa ifanye safari yake toka Songea kwenda Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 25/5/2018 saa 12 asubuhi, kuwa safari hiyo itafanyika Jumapili tarehe 27/05/2018 saa nane mchana. Mabadiliko haya yanatokana na kuchafuka kwa hali ya hewaa angani. Jina la mtoa tangazo liwe kudura Riziki.
SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA
TANGAZO LA KATIZO LA USAFIRI WA NDEGE
Tunawatangazia abiria wetu kuwa, ndege namba TY JET 343 haitafanya safari yake siku ya tarehe 25/05/2018 saa 12 asubuhi na badala yake itafanya safari siku ya Jumapili tarehe 27/05/2018 saa nane mchana.
Mabadiliko hayo yanatokana na kuchafuka kwa hali ya hewa angani hivyo si salama kusafiri siku hiyo. Pia, tunawaomba radhi watu wote kwa usumbufu uliojitokeza ambao kusema kweli uko nje ya uwezo wetu.
Kudura Riziki
Afisa habari shirika la ndege Tanzania