Matokeo ya NECTA Kidato cha Sita 2020 | ACSEE Results 2020

 

Mwalimu Makoba logo

Haya ni matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2020. Matokeo haya, yanakusanya masomo yote ya tahasusi za kidato cha sita nchini Tanzania. Katika matokeo haya, wanafunzi wengi wamefanya vizuri. Wachache wamefanya vibaya na wanayo nafasi ya kurudia tena kama watahiniwa wa kujitegemea. Unaweza kuyatazama matokeo hayo hapo chini.

Form Six Results 2020

Ushauri kwa mwanafunzi aliyekosa D moja ili aende Chuo Kikuu

Umepata D moja  hivyo unadaiwa D nyingine ili uweze kwenda Chuo Kikuu, usijiite umefeli, umefaulu, ila bado unadaiwa D moja.

Inawezekana kilichokufanya upate matokeo hayo ni: 

Kuchelewa kuanza masomo, 

kukosa muda wa kujisomea, 

kushindwa kufanya mitihani mingi ya kujiandaa, 

kukosa vitabu sahihi na  la siku zote: kuchanganya namba za maswali.

Kwa matokeo yako, unaweza kusoma diploma, hata hivyo, siyo sawa kusoma diploma kwa sababu hukupata D moja.

Rudia tena masomo mawili, huwezi kukosa D moja katika masomo hayo.

Utakaporudia tena, hakikisha mwalimu anakutajia vitabu sahihi unavyotakiwa kuwa navyo, na hakikisha unakuwa navyo vitabu hivyo.

Kwa kuwa tayari ulishasoma, tumia muda mwingi kujipima kufanya mitihani na mwalimu akusahihishe neno kwa neno.

Usajili ukianza, jisajili tena, huwezi kukosa D iliyobaki.

Forward Katika Magroup Iwasaidie Wengi Zaidi.

#MwalimuMakoba

Tazama Hapa Huduma Zetu

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie