Kanuni Kumi za Maisha Ambazo Hazisemwi Sana

Madereva wa vyombo vya kasi.

     1.   Mtu akikuonesha picha moja katika simu yake, usiweke picha nyingine

Pia usimwombe ruhusa ya kutazama picha zingine, ishia hiyo moja labda aamue kukuonesha picha zingine kwa hiyari yake.

     2.   Kabla hujafanya kazi yoyote, kakojoe kwanza

Haijalishi ni kazi gani, nenda kajiweke sawa. Ipo siku utanishukuru kwa ushauri huu.

     3.   Ukiazima gari, irejeshe ikiwa imejaa mafuta

Hii itamfanya aliyekuazima ajivunie kukuazima. Lakini, itampunguzia hasara aliyoingia wakati anakuazima gari lake, pengine wakati anakuazima gari hilo lilikuwa na mafuta. Ni dalili njema kurejesha gari likiwa limejaa mafuta.

     4.   Usiweke mziki kwa sauti kubwa ukiwa katika kundi la watu

Siyo kila mtu anataka kusikiliza unachosikiliza. Usiwe kero, tumia spika za masikio.

     5.   Kuna wakati haupo sahihi

Siyo vibaya kukosea. Tambua kuwa umekosea, kubali na jifunze kupitia makosa yako.

     6.   Usifanye maigizo katika msiba

Wamefiwa na mpendwa wao. Usiwakwaze tafadhali, kuwa mpole na kama huwezi kutulia, rudi nyumbani haraka.

     7.   Unapotafuna, funga mdomo wako

Ni ajabu kuwa, watu wengi hutafuna midomo ikiwa wazi. Siyo tabia nzuri, funga mdomo wako kisha tafuna.

     8.   Ukiazima kitu kwa mara ya tatu, nunua chako

Ukiazima kitu kwa mara ya tatu maana yake ni kwamba, una kihitaji sana kitu hicho. Hivyo nunua chako, itakusaidia.

     9.   Usichungulie katika vipande vya mlango wa bafuni

Tabia mbaya hii. Unataka kuona nini? Tafadhali, nenda zako kwa amani, usifikiri kufanya jambo hili.

     10.               Heshimu kila mtu

Wote ni watu, wote ni binadamu. Heshimu kila mtu bila kujali chochote, ukifanya hivi, mafanikio ni yako.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie