Hoja za Kisaikolojia Zinazoshangaza Kuhusu Mwanadamu

Nilikuwa natembea katika shamba la mizabibu nikiwa na mwanafunzi wangu mdadisi. Japo tulikuwa katika shamba la mizabibu, hakutaka kufahamu lolote kuhusu mizabibu.
Mwalimu, ni yapi mambo ya kushangaza kuhusu mwanadamu?” aliuliza.
“Yapo mengi, miongoni mwayo ni haya:” nilijibu, kisha nikataja mambo 12 ya kushangaza kuhusu mwanadamu.
1. Mtu mwenye akiri nyingi, hufikiri haraka na mwandiko wake huwa mbaya. Hata hivyo, siyo kila mwenye mwandiko mbaya ana akiri nyingi.
2. Hisia zetu, kama kujisikia vibaya au hasira, zinasababishwa na jinsi tunavyowasiliana na watu wengine.
3. Jinsi mtu anavyowafanyia wafanyakazi katika mgahawa wa chakula, ndiyo sifa na tabia yake hata katika maeneo mengine.
4. Wanaume siyo wacheshi kuwashinda wanawake. Wanawake ni wacheshi zaidi na ni rahisi kuwateka watu wawasikilize.
5. Kusikiliza mziki kunakufanya utulie na kukuongezea furaha. Hivyo pale unapohisi umekosa furaha, sikiliza muziki.
6. Kufanya vitu vinavyokutisha, hukufanya uwe na furaha. Vitu vya kutisha vinaweza kuwa mtihani, biashara mpya na vingine vingi.
7. Watu wenye akili nyingi huwa na marafiki wachache. Watu wa kawaida huwa na marafiki wengi. Watu wenye akiri nyingi huwa na marafiki wachache kwa sababu huwa wana kawaida ya kuchagua watu wa kufanya nao urafiki.
8. Watu huvutia pale wanapozungumza kuhusu mambo wanayoyapenda. Jaribu leo kuzungumza kuhusu jambo unalolipenda uone mabadiliko.
9. Wanawake wenye marafiki wengi wa kiume huwa na furaha kuliko wenye marafiki wengi wa kike. Ninaposema marafiki, namaanisha marafiki wa kawaida, wale wa kuongea nao tu.
10. Kusafiri huimarisha afya ya ubongo na hupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la moyo na msongo wa mawazo. Safiri masafa marefu angalau mara moja kwa mwaka, nenda kwenu kasalimie, using’ang’anie mjini, ipo faida katika kusafiri.
11. Watu wanaojaribu kumfurahisha kila mtu, huishia kuwa wapweke.
12. Waharifu wanauwezo mkubwa wa kutambua kiwango cha hudhuni alichonacho mtu.
Nilimaliza kutaja mambo hayo, kisha nikakwea katika mti mmoja wa mzabibu ili nizifaidi zabibu zikiwa hukohuko juu. Yeye alibaki chini akiniombea dua kali nisiporomoke huko juu.


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne