Kanuni Tatu Muhimu Zitakazokufanya Uishi Maisha Bora

Mwanaume mwenye furaha.

1. Tazama vitu vinavyokuzunguka

Kila unapokuwa peke yako, tazama vitu vilivyokuzunguka. Tazama jinsi watu wanavyotembea, wanavyofanya hiki na kile. Tazama jinsi magari yanavyo ondoka, pia, sikiliza sauti zinazosikika mahali hapo.
Fanya haya kwa sababu:
A. Hutafikiria vitu ambavyo si vya muhimu. Akili yako itakuwa ‘bize’ kiasi cha kuondoa msongo wa mawazo.
B. Utajifunza jinsi dunia inavyofanya kazi. Inaweza kukusaidia kuwasaidia wengine, kupitia kutazama unaweza kugundua uwepo wa mawingu na kuwapa taarifa wengine juu ya uwepo wa mvua muda mfupi ujao.
C. Inakufanya uwafahamu watu haraka, pia inasaidia kuokoa muda.

2. Mpende kila mtu

Mheshimu kila mtu. Fanya hivi bila kujali kabila la mtu, jinsia au wapi anatokea. Faida za kufanya hivi ni:
A. Utaweza kusaidiwa na watu pale utakapopata shida. Mtu anayewapenda na kuwaheshimu wengine, huweza kusaidiwa wakati wa matatizo na watu wasikiapo kapata shida, husikitika na kujitolea kumsaidia. Mtu asiyewapenda wengine wala kuwaheshimu, apatapo matatizo, watu husema, ‘mwache akome.’
B. Utakuwa mwenye furaha katika maisha yako. Endapo unapenda watu na kuwaheshimu, maana yake hakuna kinyongo ndani yako. Kama hupendi watu wala kuwaheshimu utakuwa na vinyongo vingi ambavyo vitakufanya ukose furaha katika maisha yako.
C. Utaweza kupata maarifa kutoka kwa watu mbalimbali ambao una waheshimu na kuwapenda.

3. Washauri watu wengine

Faida ya kufanya hivi ni:
A. Itakusaidia uwe na busara zaidi. Mtu anapotoa ushauri humfanya hata yeye mwenyewe afaidike na huo ushauri, pia, mtu anayeshauri wengine, hujitahidi kutafuta maarifa zaidi ili aweze kuaminiwa na watu hao.
B. Utaokoa maisha ya watu wengi. Kuna watu hukata tamaa hata kutamani kujitoa uhai kwa sababu ndogo tu. Ukiwashauri wengine, huenda ukaokoa maisha ya mtu fulani, inawezekana, huwezi jua.
Hayo ndiyo mambo matatu yatakayokufanya uwe na maisha ya furaha, mafanikio, na kila lililo jema. Ukizingatia hayo, maisha yako yatabadilika mara moja. Unasubiri nini kuanza kuyafanyia kazi, usitafute sababu za kushindwa, amua sasa.
Zaliwa upya.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne