Jinsi ya Kufaulu Mtihani kwa Wanafunzi Wanaorudia
Na: Mwalimu Makoba
“Kitabu hiki ni kwa wanafunzi wanaorudia mitihani yao. Hata hivyo, kinawafaa wanafunzi walio shule, kwani mbinu zilizotajwa hazibagui!”
Utangulizi
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa na wanafunzi wanaorudia mtihani juu ya jambo la kufanya ili waweze kufaulu. Nikiwa nimesoma madarasa yote nchini Tanzania, vidato vyote vya Tanzania na miaka mitatu ya chuo kikuu iliyonipatia shahada ya ualimu, nina majibu ya swali hili.
Mwanafunzi anayerudia mtihani ni yule ambaye alikwisha fanya mtihani wake lakini kwa bahati mbaya akafeli. Lengo la kurudia mtihani huwa ni kutaka kufaulu, kuwa na vyeti ili apate uhalali kazini, kutaka kujiendeleza katika ngazi mbalimbali za masomo na wengine hutaka sifa za kusoma kozi fulani. Zipo sababu nyingi za kurudia mtihani, sitazitaja zote.
Bahati mbaya ni kwamba, wanafunzi wanaorudia mtihani ndiyo wanaoongoza kwa kufeli ukilinganisha na wale walio shuleni. Yapo mambo yanayowafanya wanafunzi wanaorudia mtihani washindwe tena na tena katika mitihani yao miongoni mwa mambo hayo ni muda na kushindwa kujua sababu iliyowafanya wakafeli.
Hapana shaka ndiyo sababu wanafunzi wengi wanaorudia mtihani wamekuwa wakishindwa mara zote. Wapo waliorudia zaidi ya mara nne au zaidi ya hapo na mambo yakawa yaleyale, hakuna kufaulu!
Vitabu vingi vinavyoeleza namna ya kufaulu mtihani, vinawazungumzia zaidi wanafunzi walioko shule na kusahau kuwa, mwanafunzi aliye shule na anayerudia wanatofauti kubwa. Mbinu zao hazifanani na hata zikifanana, utekelezaji ni tofauti.
Nimefundisha wanafunzi wengi wanaorudia mtihani na wakafaulu mara moja kwa kutumia mbinu zilizomo katika kitabu hiki. Ni mbinu zinazofanya kazi, huna haja ya kukata tamaa na kujiona wewe huna uwezo wa kufaulu, ama labda huna akili. Unachotakiwa ni kusoma kitabu hiki.
Ukweli ni kwamba, kila mwanadamu anauwezo wa kufaulu endapo tu atazingatia misingi ya mambo mbalimbali. Huna sababu ya kukosa vyeti unavyovitaka, huna sababu ya kushindwa kujiendeleza kielimu, huna sababu ya kuitwa mjinga, pia huna sababu ya kufukuzwa kazi kwa sababu huna vyeti!
Nunua nakala ya kitabu hiki kwa shilingi 5,000/= tu za kiTanzania. Kitabu kitatumwa katika mfumo wa PDF na utakuwa na uwezo wa kukisoma kwenye simu yako au kompyuta. Endapo unapata shida katika link hapo chini, wasiliana moja kwa moja na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21/ 0653 25 05 66.