Posts

Showing posts from July, 2018

Jinsi ya Kuandika Barua ya Kirafiki

Image
SHULE YA SEKONDARI SAMATA, S.  L.P 700, DAR ES SALAAM. 09/07/2018. Mpendwa rafiki, Habari yako, natumaini unaendelea vyema huko nyumbani Makete. Mimi pia ni mzima wa afya. Madhumuni ya kukuandikia barua hii, ni kutaka kukufahamisha juu ya maandalizi yangu ya mtihani wa kidato cha nne ambao ninakwenda kuufanya ifikapo tarehe tano Novemba. Nimejiandaa vyema katika masomo yote na ninatumaini nitafaulu vyema. Pia, nimepitia mitihani yote ya taifa iliyopita na nimeona jinsi maswali yanavyotoka. Mbali na hayo, nimekuwa nikijipima kwa kufanya mitihani mbalimbali na matokeo yangu ni mazuri sana. Basi rafiki naomba nikutakie kila la heri katika maisha yako hapo Makete. Nisalimie wote wanaonifahamu. Rafiki yako, Kijoto Bohari.

Maswali Mbalimbali ya Kiswahili na Majibu yake

Image
Nimekuwa nikiulizwa maswali mbalimbali na wanafunzi, nami nipatapo muda, huyajibu maswali hayo. Kwa kuwa ni maswali yanayoulizwa sana, pengine hata wewe ukawa unatafuta majibu yake. Twende pamoja. Baadhi ya majibu yamejibiwa kwa lugha ya mkato ili kuokoa muda! 1. Vigano ni nini? tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "umdhaniaye ndiye kumbe siye." Vigano ni hadithi fupifupi zinazosimuliwa kwa lengo la kueleza makosa au maovu ya watu fulani ili kutoa maadili mema yanayofaa kwa wanajamii. Masimulizi ya vigano mara nyingi hutumia methali kama msingi wake wa maadili. Methali hiyo ndiyo hujengewa masimulizi yanayolenga kumwonya mwanajamii anayetenda kinyume na maadili ya jamii yake. UMDHANIAYE NDIYE KUMBE SIYE Mzee Magani alimwamini sana mke wake, hakudhani siku moja angekuja kumfanyia unyama. Alimpenda na kumjali sana, alisahau msemo wa wahenga kuwa, umdhaniaye ndiye kumbe siye. Siku moja akiwa katika harakati za maisha za kila siku, alikumbuka kuwa am...

Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne| Pre Necta 19

Image
Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu Makoba, zingatia mambo haya: 1. Mtu yeyote na kokote aliko anaruhusiwa kufanya mtihani huu. 2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi. 3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21. 4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho. 5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili) tu. Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Makoba) “Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!” Mwalimu Makoba, Mwalimu wa Walimu na Wanafunzi, Mwalimu wa Ushindi! Sasa fanya mtihani wako… Sehemu A (Alama 10) Ufahamu Jibu maswali yote kat...