Uhakiki wa Diwani ya Wasakatonge| Kidato cha Tatu na Nne

Uhakiki wa Diwani ya Wasakatonge| Kidato cha Tatu na Nne

JINA LA KITABU; WASAKATONGE
MWANDISHI; MUHAMMED SEIF KHATIB
MCHAPISHAJI; OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA; 2003

Utangulizi

Wasakatonge ni diwani inayozungumzia hali ngumu ya maisha. Matatizo anayoyataja mshairi ni magumu kutibika mfano wa saratani, hata hivyo wananchi wakiungana na kupambana pamoja jamii mpya yenye misingi ya usawa itapatikana.

Maudhui
Maudhui yamejengwa na vipengele vidogo kama;

Dhamira

1. Uongozi mbaya

Jamii nyingi za kiafrika zinakabiliwa na suala la uongozi mbaya. Wapo viongozi ambao hawataki kuachia madaraka kama ilivyooneshwa katika shairi la MADIKTETA,
“Mizinga nayo mitutu,
 haitoi risasi,
hutoa maraisi,
walio madikteta.”
Ni ukweli kuwa viongozi madikteta ndio chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika bala la Afrika.

2. Matabaka

Migogoro mingi inaibuka katika jamii kati ya tabaka la wenye nacho na tabaka la wasionacho katika kugombea mahitaji ya kila siku. Katika shairi la TONGE LA UGALI, mshairi anasema,
“wanapigana,
waumizana,
wauwana,
kwa tonge la ugali.”
Tunaoneshwa kuwa tabaka masikini linajaribu kupambana na tabaka tajiri ili liweze kupata tonge la ugali.

3. Umasikini

Mshairi amejadili kwa kina kuhusu tatizo la umasikini, katika shairi la WASAKATONGE, anaonesha jinsi ambavyo masikini wanavyotokwa jasho kwa sababu ya kufanya kazi ngumu zenye mishahara ya kijungujiko.
“jua kali na wasakatonge,
wao ni manamba mashambani,
ni wachapakazi viwandani,
lakini bado ni masikini.”
Wasakatonge wanafanya kila jitihada ili waweze kujinasua kutoka katika umasikini lakini inashindikana na jasho linaendelea kuwatoka.

4. Mmomonyoko wa maadili

Dhamira hii imejadiliwa katika shairi la JIWE SI MCHI. Mshairi anakemea tabia ya wanawake wanaooana wao wenyewe kana kwamba wanamume wamekwisha. Mshairi anayalaani mambo haya mapya yanaingia taratibu na kutaka kuharibu tamaduni zetu.

Ujumbe

1. Uongozi mbaya ndiyo chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika bara la Afrika. Ujumbe huu unapatikana katika shairi la MADIKTETA.

2. Uhusiano wa unyonyaji umesababisha matabaka na masikini ndiye anayeumia. Haya yamejadiliwa katika shairi la TONGE LA UGALI.

3. Umasikini ni tatizo sugu katika jamii. WASAKATONGE.

4. Viongozi wengi hubadilika kama vinyonga hivyo katika uchaguzi, wapigakura wawe makini. VINYONGA.

Msimamo

Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi anashauri kuwa, ili kuondoa matatizo yanayojitokeza katika jamii, lazima jamii ifuate misingi ya usawa na haki kwa wote.

Falsafa

Mwandishi anaamini kuwa, jamii yenye maendeleo, ni ile inayofuata misingi ya haki na usawa.

Fani

Muundo

Mwandishi ametumia miundo hii:

Tathlitha

Ni muundo ambao ubeti mmoja huwa na mistari mitatu.
Mfano wa mashairi yaliyotumia muundo huu ni “Nilinde”, “Tutabakia wawili”, “Itoe kauli yako”, “usiku wa kiza” na “Sikujua”.

Sabilia

Muundo huu hutumia zaidi ya mistari mitano katika ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia muundo wa sabilia ni: “Waso dhambi”, “Sikuliwa sikuzama”, “Madikteta”,“Si wewe?”,“Vinyonga”

Tarbia

Huu ni muundo unaopedwa na washairi wengi, mistari minne katika ubeti, ndiyo sifa yake.
Mfano ni shairi la “Mahaba”, “Machozi ya dhiki”, “Mcheza hawi kiwete”, “Sivui maji mafu”.

Mtindo

Mwandishi ametumia mitindo yote miwili: mtindo wa kimapokeo na mtindo wa kisasa.

Baadhi ya mashairi ya kisasa ni: “Sikujua”, “Tutabakia wawili” na “Jiwe si mchi”
Baadhi ya mashairi ya kimapokeo ni: “Mahaba”, “mcheza hawi kiwete” “Sivui maji mafu” na mengine.

Matumizi ya Lugha

Vipengele vya matumizi ya lugha vinajadiliwa.

Tamathali za semi

Tashibiha

“lnanuka kama ng’onda” – “Kansa”

Sitiari

“Usijigeuze Popo” – “Itoe kauli yako”
“Uchoyo ni sumu” – “Pendo tamu”

Tashihisi

“Inaumwa Afrika” – “Tiba isotibu”
“Radi yenye chereko” – “Afrika”
“Pendo lenye tabasamu” – “Pendo tamu”

Mubaalagha

“Pendo tamu kama letu duniani hulikuti” – “Pendo tamu”.

Mbinu nyingine za kisanaa

Takriri

Mfano “nilikesha”- “nilikesha”
“Buzi” – “Buzi lisilochunika”

Matumizi ya semi

Misemo

“mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao” – “Mcheza hawi kiwete”

Ujenzi wa taswira

“Vinyonga” – “viongozi wasaliti” – “vinyonga”
“Chui na Simba”- “watu wenye mamlaka” – “miamba”
“Bundi” – wakoloni wanyonyaji” – “Bundi”
“Vindama”- “nchi zinazoendelea” – “fahali la dunia”.
“Fahali la dunia” – “nchi za ulaya”

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie