Uhakiki wa Diwani ya Wasakatonge | Kidato cha Tatu na Nne
JINA LA KITABU; WASAKATONGE MWANDISHI; MUHAMMED SEIF KHATIB MCHAPISHAJI; OXFORD UNIVERSITY PRESS MWAKA; 2003 Utangulizi Wasakatonge ni diwani inayozungumzia hali ngumu ya maisha. Matatizo anayoyataja mshairi ni magumu kutibika mfano wa saratani, hata hivyo wananchi wakiungana na kupambana pamoja jamii mpya yenye misingi ya usawa itapatikana. Maudhui Maudhui yamejengwa na vipengele vidogo kama; Dhamira 1. Uongozi mbaya Jamii nyingi za kiafrika zinakabiliwa na suala la uongozi mbaya. Wapo viongozi ambao hawataki kuachia madaraka kama ilivyooneshwa katika shairi la MADIKTETA, “Mizinga nayo mitutu, haitoi risasi, hutoa maraisi, walio madikteta.” Ni ukweli kuwa viongozi madikteta ndio chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika bala la Afrika. 2. Matabaka Migogoro mingi inaibuka katika jamii kati ya tabaka la wenye nacho na tabaka la wasionacho katika kugombea mahitaji ya kila siku. Katika shairi la TONGE LA UGALI, mshairi anasema, “wanapigana...