Tanzania Kifua Mbele, Yatofautiana na Kauli ya Donald Trump

Tanzania Kifua Mbele, Yatofautiana na Kauli ya Donald Trump
Siku chache zilizopita, Donald Trump ambaye ni rais wa Marekani alitoa kauli tata ambayo ilikutana na ukosoaji mwingi zaidi kuwahi kutokea. Trump alidai anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israel.
Baada ya nchi nyingi ikiwemo Saudi Arabia kupinga kauli hiyo, Tanzania nayo imejitokeza hadharani na kutofautiana nayo.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema inaunga mkono makubaliano ya kimataifa ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina ya kumiliki mashariki wa Jerusalem kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967.
Taarifa iliyotiwa saini na Waziri Mahiga ilisema, “Tanzania inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya mataifa mawili ambayo unatoa nafasi ya Israel na Palestina kuwepo kwa pamoja zikiwa na mipaka salama."
Msimamo wa Tanzania unakwenda pamoja na msimamo wa mataifa mengi ulimwenguni.
Kauli ya Trump imetajwa na wachambuzi wengi kuwa ni yenye utata na inayoweza kusababisha kukosekana kwa amani zaidi katika eneo la Israel na Palestina.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne