Kauli ya Trump Yazua Utata, Yatajwa Kuvuruga Amani
Wakati mgogoro wa Marekani na Korea ya Kaskazini ukiwa
bado unarindima, tishio jingine limeibuliwa na kauli tata aliyoitoa rais Trump
siku chache zilizopita.
Katika kauli hiyo, Trump amenukuliwa akisema kuwa,
anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israel.
Tayari wapalestina wamenza kuchoma moto picha za Trump
kwa madai ya kukasirishwa na kauli yake hiyo.
Nayo Saudi Arabia imelaani hatua ya Marekani kuutambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Katika taarifa yake, taifa hilo limesema
kitendo hicho si cha haki.
Mgogoro wa Israel na Parestina umedumu kwa miongo
kadhaa huku Marekani na Uingereza zikitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya
mgogoro huo.
Pande zote mbili, Palestina na Israel zimeendelea
kuung’ang’ania mji wa Jerusalem kwa sababu mji huo una historia kubwa katika
imani ya Kikristo na Kiislamu.
Wachambuzi wa siasa za Palestina na Israel wameonya
kuwa, kauli ya Trump inaweza ikasababisha umwajikaji wa damu kuliko
inavyotarajiwa.
Chanzo cha mgogoro wa Palestina na Israel, historia ya
jamii hizo na imani tofauti za kidini zinafanya iwe vigumu kutoa suruhu.