UTAFITI MPYA WA TABIA ZA NGONO WAJA NA MAJIBU YA KUSHANGAZA!

UTAFITI MPYA WA TABIA ZA NGONO

Utafiti mpya kuhusu tabia za ngono umefanyika na kuja na majibu ya kushangaza. Utafiti huo uliofanywa nchini Uingereza umeeleza kwamba, wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa ikilinganishwa na wanaume.
Chanzo kikubwa kilichoeleza kusababisha wanawake kupoteza hamu ya tendo la ngono, ni kuishi kwa muda mrefu na waume zao. Kwa wanaume kinachosababisha kupoteza hamu ya tendo la ndoa ni umri mkubwa.
Jambo jingine ambalo linaweza kuathiri hamu ya tendo la ngono kwa wapenzi wote wawili ni hali mbaya ya kiafya.
Watafiti hao wamekuja na majibu kuwa, tiba pekee kwa mtu mwenye matatizo hayo, siyo dawa bali ni kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kulibaini tatizo.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na BMJ open, wanaume wenye umri wa miaka 35 mpaka 44 hukumbwa na tatizo la kupoteza hamu ya tendo la ndoa, huku kwa wanawake wakionekana kukumbwa na tatizo hilo wakiwa na umri wa miaka 55 mpaka 64.


POVU LA MWALIMU MAKOBA KWA WASANII WANAOVAA HOVYO...

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu