ROONEY KICHWA NGUMU, AVUNJA SHERIA ZA NCHI YAKE
![]() |
Rooney ndani ya gari lake |
Mshambuliaji wa Everton,
Wayne Rooney, amejikuta matatani baada ya kuangukia mikononi mwa polisi. Wanausalama
hao wamesema mwanasoka huyo alikamatwa siku ya Ijumaa kwa kosa la kuendesha
gari akiwa amelewa jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Uingereza.
Rooney ambaye anashikilia
rekodi ya kuwa na magoli mengi katika timu yake ya zamani ya Manchester United,
alikamatwa na Polisi karibu na nyumbani kwake huko Cheshire.
Huu ni mwendelezo wa makosa ya staa huyo wa soka kwani siku chache zilizopita aliingia mikononi mwa polisi
kwa kosa la kuendesha kwa mwendo mkali zaidi ya viwango vilivyowekwa.
Ukiachilia mbali kesi hizo,
mwanasoka Rooney ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa aliyoipatia mafanikio makubwa ikiwemo kuifungia magoli 53 katika michezo 119
aliyocheza.
NA: MOWASHA| NGEME