MAREKANI YAKUMBWA NA BALAA JINGINE

Misukosuko imezidi kuiandama nchi
ya Marekani. Baada ya kuibuka kwa matukio mengi ndani ya kipindi cha muda mfupi
ikiwemo mashambulizi ya kigaidi, hatimaye janga jipya limechomoza.
Kimbunga kinachotambulika kwa
jina la Irma kinatajwa kupiga kisiwa cha Marco huko Pwani ya Florida.
Upepo wake ni hatari na unakadiliwa kuwa na kasi ya Kilomita 192 kwa saa. Hata hivyo, kimeelezwa kushuka na huenda hali ikawa shwari.
Upepo wake ni hatari na unakadiliwa kuwa na kasi ya Kilomita 192 kwa saa. Hata hivyo, kimeelezwa kushuka na huenda hali ikawa shwari.
Hasara ya kuanguka na kuharibika
kwa majengo zaidi ya milioni 3.4 na kukosekana kwa umeme ni miongoni mwa maafa
yaliyolikumba jiji la Florida.
Vifo vitatu vimetajwa
kusababishwa na kimbunga hicho. Pia huenda kikaendelea kufanya uharibifu mkubwa
zaidi.