KAULI HII YA KOREA KASKAZINI KWA MAREKANI, INAHATARISHA AMANI YA DUNIA

ugomvi wa korea ya kaskazini na marekani

Korea ya Kaskazini imetoa kauli nzito ambayo inaweza kuhatarisha amani ya dunia na kusababisha vita kubwa kuwahi kutokea katika historia ya mwanadamu.
Balozi wa nchi hiyo, Han Tae Song akiwa katika kikao cha Umoja wa Mataifa amesema, 
“Hatua zitakazochukuliwa na Korea Kaskazini zitaisababishia Marekani machungu makali ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika historia yake.”
Maneno hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo kadhaa ikiwemo kupigwa marufuku uuzwaji wa mafuta na bidhaa kwenda nchi hiyo.
Mapema mwezi huu, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la sita la kombora la nyuklia ambalo linatajwa kuwa kubwa zaidi. Ufanyaji wa majaribio wa makombora ya Nyuklia unaifanya nchi hii iwe na migogoro ya mara kwa mara na mataifa mengi ikiwemo Marekani.

Endapo mgogoro huu wa Marekani na Korea Kaskazini hautatafutiwa suluhisho, huenda dunia ikashuhudia vita kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mwanadamu.

TAZAMA POVU LA MWALIMU MAKOBA KWA WASANII WAVAA HOVYO...

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne