DIAMOND KIBOKO, KAELEZA KILA KITU KUHUSU MOBETO
Lile fumbo la muda mrefu kati ya
Diamond na koo asiyeishiwa vituko Hamisa mwana wa Mobeto leo limefumbuliwa
mchana kweupe! Sekeseke hilo lilianza wakati Hamisa akiwa mjamzito ambapo
zilipatikana habari za chini kwa chini kuwa mimba hiyo ni ya mtu mzima Dangote.
Fukuto lilishamiri zaidi baada ya
Hamisa kujifungua mtoto na kumpa jina la Abdul Nasib Abdul. Hapo watu wakakaa
mkao wa kutamani kupata habari.
HATIMAYE JIBU LIMEPATIKANA
Akizungumza leo asubuhi Radio
Clouds, Diamond alikubali kuzaa na Hamisa Mobeto ila akasikitishwa na jinsi koo
huyo anavyotamba na kumfanya ‘maza hausi’ Zari ajisikie vibaya.
Alizidi kufafanua kuwa, yuko
tayari kuhudumia malezi ya mtoto ambayo hata hivyo lazima yawe yanakubalika
kisheria.
AOMBA MSAMAHA KWA KUCHEPUKA
Katika hali isiyotarajiwa, mkali
wa Zilipendwa aliwaomba radhi mashabiki wake kwa kuwaangusha baada ya kuzidiwa
na tamaa za mwili na kujikuta anachepuka na koo mwenye vurugu nyingi mjini.
Akiongea kwa msisimko alieleza
kuwa anampenda sana mwandani wake, Zari na anajutia kwa yote yaliyotokea.
PICHA YA MTOTO
Picha ya mtoto tayari
imesharushwa katika ukurasa wake wa Instagram na watu wanatoa maoni yao
mbalimbali ikiwa ni mseto wa matusi na hekima za walimwengu.
Na: Daud Makoba
Shusha maoni yako kuhusu
varangati hili…