MECHI YA CHELSEA NA BURNEY: MORATA AU BATSHUAYI?
![]() |
Uwanja unaomilikiwa na timu ya Chelsea - Stamford Bridge. |
Baada ya kuipiga Arsenal
mabao matatu kwa nunge katika mchezo wa kupasha misuli kabla ya ligi kuanza, na
baadaye kupoteza michezo mitatu mfululizo dhidi ya: Bayern Munich, Inter Milan
na The ‘Gunners’, kocha Antonio Conte hatazamii chochote ila ushindi.
Kwa upande wa timu ya pili,
Victor Moses hatacheza kwa sababu ya kadi nyekundu aliyoipata katika fainali ya
kombe la FA mwezi wa tano.
Swali linaloibuka ni nani ataziba pengo la winga wa kulia Moses? Ni lazima Conte atachagua kati ya Michy
Batshuayi au mchezaji mpya Alvaro Morata.
Hata hivyo kutokana na aina
ya uchezaji wa Morata, anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuanza.
Toa maoni yako. We unafikiri
nani ataanza?
IMEANDIKWA NA MOWASHA / NGEME
Shusha comment yako…