Kwa Nini Una Kibamia? na Jinsi ya Kuepuka Madhara Yake
NI tatizo linalosumbua vichwa vya wanaume wengi. Si wao tu, hata
wanawake walioolewa na watu wa aina hii hawaridhiki na hali, wanahisi kuna kitu
wanakosa.
Kibamia, ama uume mdogo hupimwa kwa kuangalia ukubwa wa uume uliosimama. Uume wa kawaida huanzia sentimita 12. inaweza kuwa chini ya sentimita 12 na isiwe kibamia, kwa mfano, mwenye sentimita 11, 10 au 9, bado siyo kibamia. Hivyo basi, kibamia ni uume ambao hauvuki sentimita 6.
Kwa nini una kibamia? 😯
Sababu ya kwanza ni kurithi. Watoto wanapozaliwa hurithi vinasaba kutoka
kwa baba na mama. Kama baba yako alikuwa na ‘kibamia’ basi hapana shaka yoyote
hata wewe utakuwa hivyo.
Sababu ya pili ni vyakula
ulivyokula wakati wa ukuaji wako. Vyakula vyenye sukari na protini vinamsaada
mkubwa katika ukuaji wa kiungo chako hicho nyeti. Kumbuka kwamba, huwezi
kujenga ghorofa bila kuwa na matofali. Hivyo, vyakula ni nyenzo mojawapo
inayosaidia kujenga maumbile.
Nifanye nini kuepukana na
tatizo hili? 😌
Kwanza natoa onyo. Usikimbilie kutumia madawa ya kuongeza urefu wa
mashine yako. Mazoea haya yana madhara makubwa huko mbeleni ikiwemo kupelekea
kansa au kupoteza nguvu za kiume. Njia sahihi ni kula vyakula vyenye
virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini. Pia, kufanya mazoezi kuna faida
kubwa. Hakikisha hupitishi siku bila kuuchangamsha mwili wako kwa mazoezi.
Kibamia kina madhara yoyote? 😡
Kwa kuwa kuwa na kibamia hakuna uhusiano wowote na upungufu wa nguvu za
kiume, hakuna madhara yoyote kuwa na maumbile hayo. Kinachohitajika kwa
mwanamke si ukubwa wa uume, bali ni msisimko unaosababishwa na uume uliosimama
bila kujali ukubwa wake.
Hii ni kwa sababu, sehemu zinazohitaji msisimko kwa mwanamke zipo
mwanzoni mwa uke wake.
Hata hivyo, kitendo cha kuwa na kibamia, kinaweza kukuathiri
kisaikolojia kiasi cha kuona aibu hata pale unapokuwa na mwenzi wako kumuonesha
kiwanda.
Nifanye nini zaidi? 😮
Jiamini na jikubali jinsi ulivyo. Kama nilivyosema awali, ukubwa wa uume
haumaanishi kuwa na nguvu za kutosha kumridhisha mwenzi wako, wapo watu wana
maumbile makubwa lakini hawana uwezo wa kumaliza hata nusu dakika. Hivyo,
mwanaume mzuri ni yule anayemridhisha mpenzi wake bila kujali ukubwa wa ndonga!