HII HAPA ‘TWEET’ YA OBAMA ILIYOONGOZA KWA ‘LIKES’


Hii ni Tweet ambayo imeongoza kwa kupata ‘likes’ nyingi zaidi katika mtandao wa ‘twitter’.
Katika ‘tweet’ hiyo, Obama amenukuu maneno matatu yaliyowahi kusemwa na rais  wa zamani na mpigania uhuru wa Afrika ya Kusini – Nelson Mandela. Pia ‘tweet’ hiyo, ina picha ya Obama akiwa na watoto wenye asili tofauti, wakitabasamu kwa pamoja.
Kwa sababu ya uvamizi uliotokea Charlottesville, Virginia, imepata zaidi ya ‘likes’ milioni tatu.
Picha inayoambatana na ‘tweet’ hiyo ilipigwa mwaka 2011 na aliyekuwa mpiga picha wa ikulu, Pete Souza.

‘Tweet’ hiyo inasema, ‘hakuna mtu aliyezaliwa akimchukia mtu kwa sababu ya rangi yake ya ngozi, historia au dini yake.


IMEANDIKWA NA MOWASHA/NGEME| KWA MSAADA WA MTANDAO

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie