BARCELONA YAKUMBWA NA SHAMBULIO LA UGAIDI

barcelona yakumbwa na shambulio la ugaidi
Askari wakiwa eneo la tukio
Basi dogo limeripuka katika kundi la wapita njia Barcelona, Hispania. Mlipuko huo umesababisha majeruhi na vifo kadhaa.
Askari wamesema, basi hilo limesababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 80. Vyombo vingi vya habari vimeripoti kuhusu tukio hilo.
Askari wamethibitisha kwamba, hilo ni shambulio la Ugaidi.
Waziri mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy Brey akitumia mtandao wa ‘twitter’, amewapa pole majeruhi wote na kuwataka askari wafanye kazi kwa weredi ili kuhakikisha wahalifu hao wanatiwa nguvuni.
Wamiliki wa vyombo vya usafiri wameomba kusitisha usafiri katika eneo lilipotokea shambulio na wanawaomba watu wasikae mahali hapo.
Pia, askari wamewaomba watu wote kutokutuma picha za shambulio hususani zile zinazowaonesha majeruhi.

IMEANDIWA NA: MOWASHA / NGEME



Popular posts from this blog

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

VICHEKESHO HIVI KIBOKO! SOMA KWA UANGALIFU USIVUNJE MBAVU ZAKO!