PUNDA WA MZEE BRUDA

Mzee Bruda anaye punda wa kiume ambaye anampenda sana. Punda huyu, anamanyoya meusi na meupe yaliyopangiliwa vyema hata humfanya aonekane mtanashati na nadhifu.

Punda wa Bruda hula nyasi peke yake, hupenda nyasi ndefu zilizomea vyema, amalizapo kula, hulala kwa furaha ya shibe.

Watu wengi huenda kumtazama punda wa Bruda. Wazee hutueleza kuwa hawajapata kumuona punda mwenye kuvutia kama yule. Hata hivyo waliomsogelea, aliwapiga mateke wakabaki wakigugumia kwa maumivu.


Kama nilivyosema awali kuwa, Bruda anampenda sana punda wake, punda huyu hajawahi kuadhibiwa kwa makosa yake.Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu