RIWAYA: MCHEZO WA JOGOO (sehemu ya tatu)

“Haya mzee nambie kimekusibu nini?”
          “Ooh binti yangu kwanza asante sana. Mimi bana ni mzee ninayejishughulisha na kazi ndogondogo tu.” Alijibu mzee Chekeche, kisha akakohoa kinafiki pengine kutafakari uongo uliotukuka, kisha akaendelea kuzungumza kwa simanzi la kuigiza. “Binti mimi kama nilivyokueleza, pamoja na kujishughulisha na hizo kazi, lakini pia mimi ni shabiki wa mpira na huwa ninajaribu bahati yangu kwa kubashiri matokeo. Sasa leo nilibashiri timu kumi na mbili, nilibashiri ushindi kwa Man u, Barcelona, Leicester, Burnley, Chelsea, shackle 04, Genk, Dortmund, PSG, Watford, Liverpool na Arsenal. Timu zote zilishinda kama nilivyobashiri hivyo nikakabidhiwa kitita changu cha shilingi milioni thelathini na tatu! Sasa nikiwa na bahasha iliyoja fedha…” mzee Chekeche akashindwa kuendelea kuongea, machozi yakaanza kumtoka.
          “Mzee usilie… masikini wamekupora fedha zako na nguo wamekunyang’anya, usilie mzee wangu.”
          “Asante, lakini inauma sana… aaah binti mi naishi Mtendeni hivyo tukifika nishushe tu”
          “Mzee mi naona tupitie kwanza nyumbani kwangu nikakupatie nguo za kukusitiri, sio mbali kutoka Mtendeni, naishi Mkoroshoni.”
          “Haina neno binti, naitwa Chekeche… kijana wa zamani? Vipi mwenzangu una jina?”
          “Ha ha ha… ninalo… mmmh, naitwa Suzi.”
Safari ya Suzi na mzee Chekeche iliendelea, Chekeche kwa uchovu aliokuwa nao, akasinzia, akiwa usingizini, akaanza kuyaota ‘mavituz’ aliyotoka kuyala na Mayasa, mpini wa mzee ukasimama imara, Suzi akauona. Suzi binti ambaye aliolewa na mwanaume mnene mwenye maradhi ya kisukari kilichokolea, ambaye yeye aliweza kufanya kazi za ofisini tu lakini kazi zingine hakuweza kuzifanya ikiwemo tendo la ndoa na mkewe. Inasemekana kuwa huu ulikuwa mwaka wa saba Suzi hajapewa tendo la ndoa na mumewe na hakuwahi kuchepuka, alimvumilia mumewe na aliamini ndoa ni zaidi ya tendo. Kitendo cha mpini wa mzee Chekeche kusimama, Suzi akaushuhudia, kiliamsha hamu ya miaka saba aliyokuwa nayo binti huyu asiye na hatia.


Itaendelea jumapili...


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne