Kapalalai: Mc, Mchekeshaji, Mwanamuziki… Vipaji Lukuki!

Mc kapalalai akiwa kabeba fimbo.
Ni vigumu kuzungumzia tathnia ya vichekesho bila kulitaja jina la Kapalalai kijana aliyetamba katika kipindi cha KANJANJA. Umahiri wake wa kuigiza sauti ya kimasai ndio unaomfanya azikonge nyoyo za wamsikilizao na kumtazama huku akiwaacha na kicheko kisichokuwa cha hiyari kwa jinsi anavyoweza kupangilia vioja.
Katika muziki hajalaza damu. Mtindo wake wa uimbaji naufananisha na ule wa marehemu Mr. Ebo. Hakika Kapalalai anatupunguzia machungu ya kumpoteza mzee wa kamongo. Hata hivyo, katika aina yake ya uimbaji, anaupekee wa kutosha unaomtofautisha na kumfanya awe yeye! Hiki ni kipaji kikubwa walichonyimwa wengi. Kwa sasa, anatamba na wimbo wake uitwao BISHOO na tayari amekwisha ufanyia video.
Miongoni mwa shughuli zinazotunisha pochi yake ni ‘ushereheshaji’ (MC). Amepokea na anaendelea kupokea mialiko mingi ya kusherehesha katika harusi nyingi na pengine si harusi pekee, bali shughuli yoyote inayohitaji msema chochote, Kapalalai ataifanya vyema na hutajutia kumuita. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu namba: 0718 228 972.
Yapo mengi ya kumzungumzia Kapalalai, hayawezi kuisha kwa siku moja, ila mengine unaweza kuyafahamu kutoka kwake kwa kumfuatilia katika mitandao ya kijamii: facebook, ‘Mc Kapalalai’ na instagram, ‘mckapalalai’.
Wanamuita Kapalalai handsome ya boma, MZEE WA CHEKA USIBOEKE!


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu