UTAFITI; NCHI KUWA NA MATUKIO MENGI, CHANZO KINGINE CHA AJALI ZA BARABARANI KILICHOSAHAULIKA.

Anaandika Mtafiti; Daud Makoba
Kuishi Tanzania ni kama kuishi ndani ya luninga, matukio yanapishana kwa kasi ya ajabu, likitoka hili laja lile basi vurugu mwanzo mwisho.
Ona mfululizo wa matukio haya, MAUAJI, KESI, UTUMBUAJI, VIFO VYA VIONGOZI, TETEMEKO LA KAGERA, UHAKIKI WA WATUMISHI, BUNGE LIVE, AJIRA, OPARESHENI UKUTA, FARU JOHN, KUTEKWA/KUJITEKA KWA WASANII, VITA YA MADAWA YA KULEVYA, SAKATA LA DAUDI BASHITE, BOMOA BOMOA, MVUA ZISIZOKATA, NJAA, UKAME, MKUU WA MKOA KUVAMIA KITUO CHA REDIO… yako mengi, haiwezekani kuyataja yote.
Kivipi matukio haya yanachangia kusababisha ajali za barabarani? Madereva wamegeuzwa wafuatiliaji wa matukio haya ya kusisimua. Kila kukicha wanajiuliza leo litasemwa lipi na kesho kitatokea nini? Katika kanuni za udereva, unatakiwa uweke akili yako yote barabarani, hutakiwi kufanya chochote kile isipokuwa kuendesha gari lako. Kwa kuwa udereva si sehemu ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kitendo cha madereva hawa kufikiria zaidi matukio yanayotokea nchini, kinawafanya washindwe kuweka akili yao katika safari. Kama hujatuliza akili yako katika gari unaloliendesha, basi unaialika ajali.
Rai yangu ni kwamba; wanasiasa waache kufanya mikasa, wafanye siasa. Kutamani kumulikwa na kamera za waandishi wa habari kila wakati kunaliselelesha taifa letu katika kijito kidogo chenye giza nene.
Mambo mengine yanayosababisha ajali za barabarani ni, mwendokasi, ubovu wa barabara, ulevi na rushwa za barabarani.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1