Posts

Showing posts from April, 2018

Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne| Pre Necta| 28 Apr 18

Image
Sehemu A Ufahamu (alama 10) 1.  Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata: BAADA ya kusikia simulizi mbalimbali kuhusiana na ‘chuma ulete’  kwa muda mrefu, nikaamua nijaribu ili niweze kurahisisha maisha. Nilitamani sana zile hadithi za ‘chuma ulete’ ziwe kweli juu yangu. Ninunue bidhaa kisha fedha zinirudie, zikiwa nyingi zaidi. Nile bila jasho. Baada ya mawazo hayo, siku chache zilizopita nikaamua kwenda kwa mganga mmoja wilayani Bagamoyo ambaye alisifika sana kwa kutengeneza utaalamu huo. Nilifika kwa mganga, nikavua viatu kisha nikaingia ndani. Kama kawaida mganga alinikaribisha kwa mapambio ya ‘kilozi’. Zilipigwa chafya nyingi zilizosindikiza maneno yasioeleweka. Kabla sijamweleza shida iliyonipeleka pale, mganga akaanza kubashiri: “Kijana una matatizo makubwa, mambo yako hayaendi kuna watu wanakuchezea… umekuja kumtambua anayekufanya ushindwe kupiga hatua… “ Mganga mtaalamu mlozi aliendelea kuongea mambo mengi ambayo sikuhusiana nayo, nilipoo...

History Examination for Form Four| Pre Necta| 22 Apr 18

Image
JINSI YA KUFANYA MTIHANI HUU Mtu yeyote na kokote aliko anaruhusiwa kufanya mtihani huu. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000 (elfu mbili) tu. Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 na Tigo pesa 0653 25 05 66 “Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!” Mwalimu Makoba| Mwalimu wa Waalimu na Wanafunzi| Mwalimu wa Ushindi! Unataka kufanya mtihani huu na hujaelewa taratibu zake? Wasiliana na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21. Sasa fanya mtihani wako. Tumia masaa  mawili na n...

Semantiki na Pragmatiki ya Kiswahili | KI 311

Image
Aina za Maana Maana msingi Ni maana tunayoipata katika kamusi. Ni ile maana halisi. Mfano, Kupe – mnyama anayenyonya damu. Udhaifu wa nadharia inayotokana na maana msingi i.  Inajikita katika viumbe hai tu. ii.  Inashindwa kutoa sifa za maneno dhahania. iii.  Inashindwa kutofautisha polisemia na homonimia. iv.  Inashindwa kutoa unyume wa mwanamume na mwanamke kama ni jinsi au vipi? v.  Kuna utata katika kubainisha sifa za maana husika kwani kuna baadhi ya maneno si rahisi kutambua sifa zake, mfano; la. Maana dokezi Inaweza ikatokana na maana msingi. Mfano: tabaka la juu ni majipu, mirija, kupe. Pia inatokana na mitazamo ya jamii . Wafaransa humchukulia mwanamke kama kiumbe dhaifu, hivyo magari madogo huyaita kwa kuanzia na herufi ‘la’ ikimaanisha jinsia ya kike. Mfano, anahuruma kwa sababu ni mwanamke. Maana dokezi hutokana na sifa kuu tatu i.  Sifa za kiungo cha kitu. Sifa hizi zinatokana na umbo la kitu fulani. Mfano, mwonek...