Vichekesho 10 Vinavyochekesha Mpaka Mbavu Ziume

Wanawake wawili wamekaa katika sofa, wanacheka.

Kama unataka kuwa mwenye afya bora, basi hakikisha unacheka, siku inayopita ikiwa na vicheko ndani yake ni siku bora mno.Kucheka ni jambo muhimu katika maisha. Kucheka huongeza kinga katika mwili wako, husaidia mwili kutoa homoni ya furaha aina ya ‘endorphins’, kucheka hulinda moyo, husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, hupunguza hasira na kucheka kunaweza kuongeza hata siku zako za kuishi. Leo tunakuletea vichekesho 10, ambavyo ni lazima vikufanye ucheke, ufurahi na uwe mwenye afya bora.

1. Nilikuwa na mjomba yangu, yeye alikuwa akiniambia nisiogope kitu kwa sababu ni askari. Siku moja nilikamatwa, nikampigia simu kumuita, alipofika, nikamwambia awaambie askari wenzake waniachie. Mjomba akanijibu kwa sauti ya upole, “Mjomba sina uwezo, mimi siyo askari polisi, mimi ni askari wa jeshi la wokovu kanisani kwetu, labda nikufanyie maombi.”

2. Mlio kwenye mahusiano, mkiambiwa ‘take care’ na wapenzi wenu huwa mnajibuje? Msaada tafadhali.

3. Nimeshuhudia mjomba akianguka kutoka juu ya mti, alipogundua nimemuona, akaniuliza, “Mjomba unaweza kuruka kama hivyo?”

4. Mzungu alienda kwa mganga akasema, “Mgangaaa, mume wangu wamemrogaa.” Mganga naye akajibu kwa kuiga lafudhi ya kizungu, “Kalete kuku mweupe na wao tuwarogeee.”

5. Nimemdai mlokole hela yangu akanijibu, “Utanidai sabini mara sabini.” Anamaanisha nini, au ndiyo nimedhurumiwa.

6. Kuwa bachela tabu sana, nimetumia saa mbili kutafuta dekio kumbe nimelivaa.

7. Ubahiri ni mzuri sana ila usiufanye kwenye chakula na mavazi. Maana utakonda na kupauka.

8. Upo zako ugenini halafu unasikia jikoni wanasema, "Hii mashine iliyokuja sidhani kama debe la unga litamaliza wiki."

9. Kuna muda maisha yanatupiga mpaka tunaogopa kula hela ya kula.

10. Unatumia uma na kisu ili usionekane mshamba. Unakata kiazi kinaruka mpaka mapokezi.

Tutahakikisha tunakuletea mfululizo wa vichekesho bora mara kwa mara. Vichekesho vyetu hukusanywa ama kuandikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha unacheka na umalizapo kucheka ama kuvisoma vichekesho hivi, tunakuhakikishia kwamba, utaendelea kutabasamu siku nzima. Hakikisha unakuwa mwenye furaha siku zote!

Kucheka ni Afya, Nunua Kitabu cha Vichekesho vya Kiswahili kwa Tsh. 5,000/= tu, Ucheke Siku Nzima, Ili Kununua, Gusa Hapa

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe