Posts

Showing posts with the label kiswahiliformfour

Uandishi | Kidato cha Kwanza Mpaka cha Nne

Image
Uandishi wa Insha Insha ni mfululizo wa sentensi zinazohusiana na mada inayozungumziwa au kuandikwa. Urefu au ufupi wa insha hutegemea mada husika inayojadiliwa. Muundo wa Insha Insha bora inatakiwa iwe na  muundo huu : -  Kichwa cha insha -  Mwanzo  au utangulizi  wa insha -  Kiini cha insha -  Mwisho  wa insha Insha za wasifu insha za wasifu ni isha zinazoelezea uzuri wa kitu, mtu, mahali au hali fulani. Mfano wa insha ya wasifu BAHARI YA HINDI Bahari ya Hindi ni bahari kubwa inayobeba eneo la mashariki mwa Afrika mpaka kwenda India. Nchini Tanzania, bahari ya Hindi ipo katika mikoa ya: Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Bahari hii ni miongoni mwa maliasili zenye thamani nchini Tanzania. Bahari ya Hindi huonekani ya bluu ukiitazama kwa mbali. Hii ni kwa sababu maji yake huakisi mawingu na kuifanya ionekane kama ya bluu. Hata hivyo, ukiyafikia maji yake ni meupe tena safi. Bahari ya Hindi pembezoni kabla ya k...

Jinsi ya Kuandika Kumbukumbu za Kikao| Mfano kutoka NECTA

Image
Nikiwa nimekaa katika kiti kikubwa cha kuzunguka, mbele nikitazama ugomvi wa buibui na siafu, siafu alionekana kuelemewa kiasi kifo kilimwita kwa sauti ya upole. “Mwalimu, kuna tatizo,” nilishtushwa na sauti ya mwanafunzi. “Tatizo gani?” niliuliza. “Mwalimu wa waalimu, sijui kuandika kumbukumbu za kikao, swali hili laweza toka  kwenye mtihani nikakosa alama.” “Usiwaze alama pekee, katika maisha halisi, unaweza kushindwa kuandika kumbukumbu za kikao kinachokuhusu endapo utapewa jukumu hilo. Kuna baadhi ya nchi usipoweza kuandika kumbukumbu za kikao unafungwa jela !” nilimaliza kwa utani, wote tukacheka, kisha msafara wa watu wawili kuelekea darasani ukafuatia. Jinsi ya Kuandika Kumbukumbu za Kikao Unapoandika kumbukumbu za kikao, hakikisha unazingatia mambo manne ambayo ndiyo sehemu ya kumbukumbu za kikao: 1.  Kichwa cha habari 2.  Waliohudhuria 3.  Wasiohudhuria 4.  Ajenda Ajenda imegawanyika katika mambo manne: I.  Kufungua kik...

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne

Image
Risala ni hotuba fupi iliyokatika maandishi na ambayo husomwa mbele ya mgeni rasmi ikielezea kuhusu mafanikio, changamoto na maombi ya kundi fulani. Muundo wa Risala -       Utangulizi. Katika kipengele hiki, cheo cha kiongozi (mgeni rasmi) hutajwa. Pia kundi linalowakilishwa. -       Kiini. Mafanikio ya kundi, changamoto za kundi, mapendekezo na ushauri. -       Hitimisho. Kipengele hiki hukaa shukrani. Sasa hebu tazama mfano huu wa risala: Swali; Jifanye wewe ni mwanafunzi wa kidato cha nne na umechaguliwa kuandaa risala itakayosomwa mbele ya mgeni rasmi siku ya mahafali yako ya kumaliza kidato cha nne. Andika risala utakayoisoma siku hiyo. RISALA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KWA MGENI RASMI Ndugu mgeni rasmi, waalimu, wazazi, wanafunzi wenzetu, wageni waalikwa mabibi na mabwana. Ndugu mgeni rasmi, tunayofuraha kukualika leo hii katika sherehe yetu ya mahafari haya ya kid...

Jinsi ya Kuandika Hotuba

Image
Hotuba ni maelezo ambayo hutolewa na mtu mbele ya watu kuhusu mada fulani. MUUNDO WA HOTUBA -       Mwanzo. Huu huambatana na salamu. -       Utangulizi. Hutaja watu na kuwatambulisha kulingana na vyeo vyao. -       Kati. Hiki ni kiini cha hotuba. Mawazo yote makuu hukaa hapa. -       Mwisho. Muhtasari wa yale yaliyoelezwa. Pia, msemaji hupata nafasi ya kuaga na kushukuru. Sasa tazama mfano halisi wa hotuba ambao umeandikwa kama majibu ya swali la nane mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2010. Eleza tofauti iliyopo kati ya hotuba na risala. Andika hotuba kuhusu “Maji ni Uhai.” Kwa kuwa mjadala wetu ni hotuba , risala haitazungumziwa, bali nitajikita katika kuonyesha mfano wa hotuba. MAJI NI UHAI Wanakijiji oyeeeeeeh! Ndugu Mwenyekiti wa Kijiji, ndugu Katibu wa Kijiji, Ndugu Wanakijiji wote mabibi na mabwana. Ninafurahi kusimama mbele yenu na kuzungumza. Nikiwa kama mw...

Jinsi ya kujibu maswali ya fasihi - riwaya, tamthiliya na ushairi

Image
Utangulizi Kijitabu hiki ni mwongozo wa namna ya kujibu maswali ya tamthiliya, riwaya na ushairi. Mada hii imekuwa ngumu na yenye changamoto kubwa, hapana shaka kuwa kijitabu hiki kitarahisisha ugumu huo. Katika mtihani wa mwisho wa kidato cha nne , maswali yahusuyo tamthiliya, riwaya na ushairi yanapatikana mwishoni mwa mtihani. Swali la kitabu linaweza kuwa la kueleza kwa isha fupi au kueleza kwa insha ndefu. Swali la kueleza kwa insha fupi linaweza kusema, "Fananisha kwa kutumia hoja nne wasifu wa ndani wa wahusika Mamantilie na Sekai." Katika makala hii, tunaangazia insha ndefu zenye alama 15 kwa swali moja. Mwanafunzi atakaye kisoma kijitabu hiki ataweza kujibu maswali ya tamthiliya , ushairi na riwaya. Kukisoma kitabu hiki ni kumiliki alama 45% za mtihani wa mwisho wa kidato cha nne hata kabla ya kuufanya mtihani wenyewe! Mwalimu Makoba. SEHEMU YA KWANZA; USHAIRI Kama wasemavyo Mlokozi na Kahigi (1982;25), ‘ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kw...