Posts

Showing posts with the label kiswahiliformthree

Utungaji wa Kazi za Fasihi Andishi | Kiswahili Kidato cha 3

Image
Utungaji ni namna au jinsi ya kupangilia visa na matukio katika maandishi kwa lengo la kuburudisha, kuelimisha na kuakisi hali ya maisha ya jamii inayohusika. Hadithi fupi Hadithi fupi ni masimulizi ya kubuni yanayosawiri tukio, tabia, mgogoro au kipengele cha maisha. Hadithi fupi huwa na tukio moja au mawili na hutumia mawanda finyu. Hadithi fupi huwa na wahusika wachache na huandikwa kwa muda mfupi. Baadhi ya fani zilizochangia kuibuka kwa hadithi fupi ni: ngano, hekaya, visasili, michapo na tendi. Katika kutunga hadithi fupi, sharti upendekeze visa vya kutungia. Mfano wa visa hivyo ni kisa cha jogoo kuwa na kishungi au kisa cha twiga kuwa na shingo ndefu. Mfano wa hadithi fupi PURUKUSHANI USIKU WA MANANE Ilikuwa usiku wa siku ya Jumatano, Mowasha alijilaza katika kitanda chake cha teremka tukaze kwa furaha kuu. Ajabu ni kwamba hakukumbuka hata kuvua viatu, alilala navyo! Kilichompa furaha Mowasha hakikuwa kitu kingine bali fedha aliyoipata baada ya kuuza pamba yake, pamba aliyohang...

Maendeleo ya Kiswahili Kidato cha Tatu

Image
Asili ya Kiswahili Zipo nadharia nyingi zinazoelezea kuhusu asili ya Kiswahili. Wengine wakisema Kiswahili ni kiarabu, pijini, lugha ya vizalia na nadharia nyinginezo. Katika nadhari hizo, nadharia inayosema kuwa Kiswahili ni Kibantu , inaelekea kuwa kweli kwa sababu imejawa na ushahidi wa kuthibitisha madai yake. Ushahidi wa kimsamiati unaothibitisha ubantu wa Kiswahili Mizizi ya msingi ya misamiati ya lugha ya Kiswahili na zile za kibantu hufanana sana. Mfano: Kiswahili Kikurya Kinyiha Kijita Maji Amanche Aminzi Amanji Jicho Iriso Iryiso Eliso Ukitazama mifano hapo juu, utagundua kuwa, mizizi ya lugha za kibantu inafanana kwa kiasi kikubwa na ile ya lugha ya Kiswahili. Ushahidi wa kimuundo unaothibitisha ubantu wa Kiswahili Muundo wa lugha za Kibantu   hufanana kwa kiasi kikubwa na ule wa lugha ya Kiswahili. Kwa mfano, namna viambishi vinavyopac...

Ngeli za Nomino | Kiswahili Kidato cha Tatu

Image
Ngeli ni utaratibu wa kuweka nomino katika makundi yanayofanana au yanayowiana. Nomino za Kiswahili zinaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali. Baadhi ya wanaisimu wamezigawanya nomino katika makundi 16 na wengine makundi 9 na wengine makundi 18. Ngeli huweza kuainishwa kwa vigezo mbalimbali. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kigezo cha upatanishi wa kisarufi au kigezo cha kisintaksia. Upatanishi wa kisarufi ni hali ya viambishi vya maneno ndani ya tungo kukubaliana na kushikamana ili kuleta maana iliyokusudiwa. Upatanishi wa kisarufi unaweza kuonekana kati ya vipashio mbalimbali vya tungo: Mifano: Unyasi umeota.    =     Nyasi zimeota. Kiazi   kitamu.   =    Viazi vitamu. Huyu mnene.    =    Hawa wanene. Huyu anakuja.   =    Hao wanakuja. Mtu ambaye.   =   Watu   ambao. Mtu aliyesafiri. = Watu waliosafiri. Aina za tungo Tungo ni matokeo ya kupanga pamoja vipashio sahili ili...