Posts

Showing posts with the label kiswahiliformtwo

Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two

Image
Nukuu za Kiswahili kidato cha pili ni:       1.    Uundaji wa maneno       2.    Matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali      3.    Uhakiki wa kazi za fasihi simulizi      4.    Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi      5.    Utungaji wa kazi za fasihi simulizi      6.    Uandishi      7.    Usimulizi      8.    Ufahamu Uundaji wa maneno ni mada ambayo inaeleza namna maneno yanavyoundwa kwa kutumia uambishaji. Mofimu nazo zimejadiliwa kwa kina. Matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali ni mada ambayo inaeleza kuhusu lugha inavyotumika katika mazingira mbalimbali. Ili kuwezesha uelewa, mada hii imejadili kwa kina masuala kama: rejesta, misimu na lugha ya maandishi na ile ya mazungumzo. Mbali na hayo, utata katika mawasiliano umejad...

Usimulizi | Kiswahili Kidato cha Pili

Image
Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Tukio hilo linaweza kutokea katika wakati mfupi uliopita au zamani kidogo. TUKIO LA MZEE NA KONDAKTA Jana nikiwa nimepanda daladala, kulitokea tukio la Mzee na kondakta wa daladala. Tukio hili lilitoka muda wa saa sita mchana. Kondakta alimfuata Mzee na kumwomba ampe nauli, Yule mzee alidai kuwa, nauli alilipa. Kondakta alidai kama mzee amelipa basi aoneshe tikiti yake. Mzee alidai kuwa, alipotoa fedha, hakupewa tikiti. Pia, mzee alitetewa na watu wengi ambao walidai walishuhudia akilipa nauli. Hata hivyo, kondakta alibaki katika msimamo wake uleule wa kumtaka Mzee alipe nauli au aonyeshe tikiti. Baada ya usumbufu kuwa mkubwa, mzee alisimama akakunja ngumi, konda naye akakunja. Mzee akarusha ngumi nzito, loooh! Konda alianguka mpaka chini. Dereva alikuja kusaidia, hata hivyo Mzee alikuwa imara, dereva alipigwa ngumi ya kichwa akadondoka hatua mbili alipodondoka konda. Dereva na konda wal...

Ufahamu | Kiswahili Kidato cha Pili

Image
Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma. Ufahamu wa kusikiliza Ufahamu wa kusikiliza, ni uwezo wa mtu kuelewa maneno anayoyasikiliza. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe. Kujibu Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha: -       Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa -       Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza. -       Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa. -    ...

Uandishi | Kiswahili Kidato cha Pili

Image
Insha za hoja Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake. Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo. Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Insha za Hoja Unapoandika insha za hoja, au aina zingine za insha, zingatia mambo haya: 1. Kubaini mada ya kuandikia insha na kuielewa vyema. 2. Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki. 3. Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la insha . Kwa mfano, mtindo wa masimulizi, unafaa kwa hadithi au insha zingine za kisanaa. 4. Kutumia lugha...