Posts

Showing posts with the label kiswahiliformfive

Ufahamu na Ufupisho | Kiswahili Kidato cha Tano na Sita

Image
Ufahamu ni kujua au kulielewa jambo hatimaye kuweza kulifafanua. Mtu anaweza akaona, akasoma, ama akasikia jambo na akaelewa au asielewe. Akielewa atakuwa na uwezo wa kufafanua au kutoa taarifa zinazohusiana na habari hiyo. Ufahamu wa kusikiliza na ufupisho Ufahamu wa kusikiliza ni ule ambao mhusika anapata taarifa hiyo kwa kusikiliza habari hiyo. inawezekana kupata habari hiyo kwa kusimuliwa au kusomewa. Ili kupata habari inayosikilizwa au inayosomwa, msikilizaji azingatie mambo haya: -       Kuwa makini kwa kila kinachosimuliwa au kinachosomwa. -       Kuhusisha mambo muhimu na habari isimuliwavyo. -       Kujua matamshi ya mzungumzaji. -       Kubainisha mawazo makuu. Kujibu maswali kutokana na habari uliyoisikiliza Mbinu za kujibu maswali kutokana na habari ya ufahamu wa kusikiliza ni: -       Kusikiliza kila swali kwa makini. -  ...

Utumizi wa Lugha | Kiswahili Kidato cha Sita

Image
Rejesta Rejesta ni matumizi ya lugha kutokana na muktadha maalumu. Siku zote, matumizi ya lugha hutofautiana kutokana na mambo mengi. Mambo ya kuzingatia unapotumia lugha Wakati unatumia lugha, kuna mambo ya kuzingatia kama yanavyoelezwa: 1. Mazingira Mazingira humwamulia mtu namna ya kutumia lugha . Kwa mfano, lugha ya hotelini ni tofauti na lugha ya kanisani. Kutokana na mazingira, tunaweza kupata lugha ya: hotelini, shuleni, ofisini, kanisani na mitaani. 2. Uhusiano baina ya wahusika Uhusiano baina ya wahusika, hufanya matumizi ya lugha yabadilike. Mfano, lugha ya marafiki vijana, imejaa misimu mingi na maneno yasiyo na adabu. Lugha ya baba na mtoto ina maneno yenye heshima. Pia, uhusiano baina ya wahusika unatupatia lugha ya mtu na mpenzi wake, mwalimu na mwanafunzi wake, meneja na wafanyakazi wa chini yake n.k 3. Mada ya mazungumzo Mada ya mazungumzo ndiyo inayokuamulia maneno ya kusema. Kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya: kibiashara, kitaaluma, mahub...