Mawasiliano | Kiswahili Kidato cha Kwanza

Mawasiliano ni kitendo cha kupashana habari. Inaweza kuwa kwa mdomo baina ya mtu na mtu, simu, barua au njia yoyote itakayosaidia kutoa habari sehemu fulani kuipeleka mahali pengine. Tunasema mawasiliano yamekamilika pale yanapoleta maana iliyokusudiwa. Jamii inayoishi watu, huwasiliana. Chombo kinachotumiwa kwa mawasiliano baina ya mtu na mtu kinaitwa lugha. Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokubaliwa na watu ili zitumike kwa mawasiliano. Lugha hujumuisha: sauti, silabi, neno na sentensi. Unapowasiliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili ni muhimu kuzingatia: kiimbo, mkazo, matamshi na lafudhi sahihi. Dhima ya lugha katika mawasiliano 1. Kupashana habari Watu hupashana habari mbalimbali kwa kutumia lugha. Habari za furaha na huzuni zote hutolewa kwa kutumia lugha. Taarifa ya habari katika redio na runinga ni mfano wa namna lugha inavyotumika kama chombo cha kupashana habari. 2. Kutambulisha mtumiaji wa lugha Kwa kusikia watu wakiwa wanazungumza, tunapata kuwafahamu watu hao ni wa ja...