Uhakiki wa riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo
Wasiliana na Mwalimu ili Kujiunga Darasa la Uhakiki wa Vitabu vyote vya Fasihi Mtaala Mpya kwa Kugusa Hapa Mwandishi: Euphrase Kezilahabi Mwaka: 1975 Mhakiki: Mwalimu Makoba Nilipofika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya masomo yangu, mtu wa kwanza kutamani kumuona alikuwa ni Profesa Euphrase Kezilahabi. Nilimsoma katika kazi zake mbalimbali ikiwamo hii ya Dunia Uwanja wa Fujo. Nilianza msako mara moja wa kumtafuta Profesa Kezilahabi bila mafanikio. Baadaye niligundua kupitia kwa mwalimu wangu M.M. Mulokozi, ambaye aliwahi kuwa mwanafunzi wa Kezilahabi kwamba, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilimfuta kazi Kezilahabi miaka mingi iliyopita! Mwishoni mwa miaka ya 1990 Kezilahabi aliomba likizo ya miaka miwili kwenda kufundisha Botswana . Alikubaliwa na akaenda Botwana mwaka 1995. miaka miwili ilipokwisha Botswana walimwongezea muda, akakiomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimwongezee muda lakini akakataliwa na kuambiwa arejee mara moja. Aliposhindwa kurejea alifutwa kazi na kujikuta ha...