Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 10,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi. CV au wasifu ni kitu cha lazima kwa yeyote anayeomba kazi. Watu wengi wanaokosa kazi, tatizo huwa siyo wao, bali tatizo huwa ni CV zao. Kumekuwa na makosa mengi katika uandishi wa CV jambo ambalo limesababisha watafuta kazi wengi kushindwa kuitwa kwenye usaili. Makala hii itakueleza namna sahihi ya kuandika CV, utaitwa katika ‘interview’ nyingi endapo utaandika CV sahihi. Tena nakukumbusha, kila taaluma ina aina yake ya CV, CV ya rubani haifanani na CV ya injinia. Vivyo hivyo, CV ya mpishi haifananani na CV ya Mwalimu. Pia nakukumbusha usome jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi , kwani CV huenda pamoja na barua ya maombi ya kazi. Hatua ya kwanza nitaonesha mfano wa CV kwa lugha ya Kiswahili na hatua ya pili nitaonesha mfano wa CV kwa lugha ya Kiingereza halafu utachagua mwenyewe utumie lugha gani katika ku