Utungaji wa Kazi za Fasihi Simulizi | Kiswahili Kidato cha 2

Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, kuna mtu alitunga kazi hizo. Mada hii, inaangazia utungaji wa kazi za fasihi simulizi: Utungaji wa mashairi Kanuni za Utungaji wa Mashairi Utungaji wa mashairi una kanuni mbili: 1. Fani 2. Maudhui Katika fani , mshairi azingatie lugha anayotumia kama: tamathali za semi, methali nahau na misemo pamoja na picha na taswira. Pia, mshairi azingatie kama mtindo wa shairi, kama ni shairi la kimapokeo au shairi la kisasa. Pia, mshairi azingatie muundo wa shairi lake, kama atatumia mistari miwili, mmoja, sita ama apendavyo yeye. Katika maudhui, unapotunga shairi zingatia wazo lako. Mfano: ni lipi lengo la wewe kutunga shairi? Inawezekana unatunga shairi ili kuzungumzia hali ya umasikini unaoikumba nchi yako, au pengine una lengo tofauti. Pia, zingatia ujumbe au mafunzo yanayopatikana katika shairi ulilotunga. Unalenga kufikisha ujumbe gani? Mfano wa shairi lililotungwa kwa kuzingatia kanuni Kubaka Nimekuwa nikipima, najiuliza k