Posts

Showing posts with the label kiswahiliformthree

Uandishi | Kidato cha Kwanza Mpaka cha Nne

Image
Uandishi wa Insha Insha ni mfululizo wa sentensi zinazohusiana na mada inayozungumziwa au kuandikwa. Urefu au ufupi wa insha hutegemea mada husika inayojadiliwa. Muundo wa Insha Insha bora inatakiwa iwe na  muundo huu : -  Kichwa cha insha -  Mwanzo  au utangulizi  wa insha -  Kiini cha insha -  Mwisho  wa insha Insha za wasifu insha za wasifu ni isha zinazoelezea uzuri wa kitu, mtu, mahali au hali fulani. Mfano wa insha ya wasifu BAHARI YA HINDI Bahari ya Hindi ni bahari kubwa inayobeba eneo la mashariki mwa Afrika mpaka kwenda India. Nchini Tanzania, bahari ya Hindi ipo katika mikoa ya: Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Bahari hii ni miongoni mwa maliasili zenye thamani nchini Tanzania. Bahari ya Hindi huonekani ya bluu ukiitazama kwa mbali. Hii ni kwa sababu maji yake huakisi mawingu na kuifanya ionekane kama ya bluu. Hata hivyo, ukiyafikia maji yake ni meupe tena safi. Bahari ya Hindi pembezoni kabla ya kuyafikia maji ina mchanga mwingi. Mchan

Uhakiki wa Diwani ya Wasakatonge| Kidato cha Tatu na Nne

Image
JINA LA KITABU; WASAKATONGE MWANDISHI; MUHAMMED SEIF KHATIB MCHAPISHAJI; OXFORD UNIVERSITY PRESS MWAKA; 2003 Utangulizi Wasakatonge ni diwani inayozungumzia hali ngumu ya maisha. Matatizo anayoyataja mshairi ni magumu kutibika mfano wa saratani, hata hivyo wananchi wakiungana na kupambana pamoja jamii mpya yenye misingi ya usawa itapatikana. Maudhui Maudhui yamejengwa na vipengele vidogo kama; Dhamira 1.  Uongozi mbaya Jamii nyingi za kiafrika zinakabiliwa na suala la uongozi mbaya. Wapo viongozi ambao hawataki kuachia madaraka kama ilivyooneshwa katika shairi la MADIKTETA, “Mizinga nayo mitutu,  haitoi risasi, hutoa maraisi, walio madikteta.” Ni ukweli kuwa viongozi madikteta ndio chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika bala la Afrika. 2.  Matabaka Migogoro mingi inaibuka katika jamii kati ya tabaka la wenye nacho na tabaka la wasionacho katika kugombea mahitaji ya kila siku. Katika shairi la TONGE LA UGALI, mshairi anasema, “wanapigana, waumizan

Uhakiki wa Diwani ya Mashairi ya Chekacheka

Image
Mwandishi;  Theobard Mvungi Wachapishaji;  EP & D.LTD Mhakiki;  Mwalimu Makoba Maudhui Dhamira 1.  Kutetea Haki Mshairi anamshauri kiongozi wa nchi aendelee kuwasha moto dhidi ya watu wote wanaodhulumu haki za wengine. Katika shairi la MWINYI UMEWASHA MOTO ANGALIA USIZIMWE, mshairi anasema, “Tumaini la wanyonge, kwamba ipo serikali, Ile nchi ya mazonge, ya wenye meno makali, Wanyang'anyao matonge, wanyonge hawana hali, Mwinyi ukiwa mkali, ndio raha ya raia.” 2.  Demokrasia Mshairi anapinga mfumo wa chama kimoja. Kwake yeye, mfumo huu, unawanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao na kukosoa pale mapungufu yanapojitokea. Shairi hili liitwalo TAIFA WAMELIZIKA liliandikwa kipindi ambacho Tanzania ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja. Hata hivyo bado lina uhalisia hasa ukizingatia uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyama vya upinzani leo hii. Mshairi anasema, “Mezikwa demokrasi, Chama kimoja ndo' ngao Watu hawana nafasi, kutetea nchi yao Mawazo ya u

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe

Image
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE MWANDISHI: EDWIN SEMZABA Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Afisa aliyetumwa kuhesabu watu-Ngoswe, anashindwa kuifanya kazi yake na kuanzisha ajenda nyingine ya mapenzi. Anapanga kutoroka na binti Mazoea aliyekwisha kuposwa tayari, Mazoea naye kusikia atakwenda kuishi mjini anakubaliana na mpango huo. Wanapotoroka, Ngoswe anasahau mkoba wenye takwimu za watu waliokwisha kuhesabiwa, Mzee Ngengemkeni Mitomingi ambaye ndiye baba yake na Mazoea, anazichoma moto takwimu hizo na kumsababishia hasara kubwa Ngoswe. J ina la Kitabu Jina la kitabu “Ngoswe penzi kitovu cha uzembe” ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii. Maudhui