Posts

Showing posts with the label kiswahiliformsix

Matumizi ya Sarufi | Kidato cha Tano na Sita

Image
Sarufi ni utaratibu wa sheria au kanuni zinazowezesha muundo wa lugha kukubalika. Matawi ya Sarufi 1.  Sarufi matamshi (fonolojia) Tawi hili la sarufi huhusu utaratibu wa mpangilio wa vitamkwa katika maneno ya lugha. Sauti zinazotolewa katika lugha ni irabu na konsonanti. Sauti hizi zinapotumiaka katika maneno ya lugha huitwa fonimu. Fonimu ni kipashio kidogo cha kifonolojia kinachobadili maana ya neno. Hivyo, tawi hili la fonolojia, limejikita katika matamshi ya maneno. 2.  Sarufi maana (semantiki) Tawi hili la sarufi hujihusisha na maana mbalimbali katika tungo. Maneno hubeba maana fulani, hivyo katika tawi hili, tunaweza kubaini maana yake. Kwa mfano: Maana ya mbuzi ni mnyama afugwaye na aliyefanana na swala. 3.  Sarufi miundo (sintaksia) Tawi hili hujihusisha na mpangilio wa maneno katika kutengeneza sentensi. Ili kupata sentensi, ni lazima kufuata mpangilio sahihi vinginevyo sentensi hiyo haitaeleweka wala kukubalika kwa watumiaji wa lugha. Kwa mfano: Mtoto M