Posts

Showing posts with the label kiswahiliformfour

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Image
TAMTHILIYA; KILIO CHETU MWANDISHI; MEDICAL AID FOUNDATION MCHAPISHAJI; TANZANIA PUBLISHING HOUSE MWAKA; 1995 JINA LA MHAKIKI; Mwalimu Daud Makoba Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia. Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa. FANI MUUNDO Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kutuonesha wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho Joti mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi. Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI. Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita. sehemu